Ukamilifu
Wangu Ufikiao Kilele Chake (My Utmost for His Hiqhest) ni kitabu bora na
maarufu kinachotumika kuamsha fikira njema za ibada ya maombi ya kila siku.
Hiki ni kitabu kinachotu patia busara ya kiroho na mwelekeo uletao
mabadiliko makuu. Mafundisho ilioko ndani yake yamegusa maisha ya mamilioni
ya watu na wameimarika katika maisha yao ya kiroho, na wakapata juhudi ya
kumfuata Mungu.
Vumbua hekima ya Oswald Chambers, mtu arnbaye anakuhimiza
ujitoe kabisa na kikamilifu kwa Mungu. Mafundisho haya ni yenye uwezo na
maono na yatauzungumuzia moyo wako, pia yatakuelekeza kwa Mungu kila siku.
Mafundisho ya Chambers huangaza upya maandiko, huku akichunguza kina cha utu
wetu, na hitaji letu kuu Ia maisha yanayornwlekea Mungu.